Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis amewateua makadinali wapya wa kanisa katoliki kote duniani, wengi ambao wanashiriki katika kumchagua mrithi wake.
Makadinali hao wapya wanatoka mabara matano akiwemo mjumbe wa Vatican nchini Syria.
Sasa Papa Francis amechagua theluthi moja wa makadinali ambao watamchagua mrithi wake.
Ni makadinali walio chini ya miaka 80 tu ambao wanaweza kumchagua Papa mpya. 13 kati ya wale walioteuliwa wako chini ya miaka 80 na sasa wanahitimu kumrithi.
Ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka mitatu ambapo Papa Franciss, ambaye ni Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini kuwateua makadinali wapya
Makadinali hao wapya wanatoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati , Bangladesh, Papua New Guinea na Mauriotius miongoni mwa nchi zingine.
No comments:
Post a Comment