AFISA MTENDAJI KATA MBARONI KWA UBAKAJI. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Sunday, November 20, 2016

AFISA MTENDAJI KATA MBARONI KWA UBAKAJI.

Afisa mtendaji wa kata ya mkuyuni Wilayani Nyamagana mkoani  Mwanza James Chiragwire (42) anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kumbaka mtoto ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nyabulogoya darasa la tatu mwenye umri wa miaka 11 jina limeifadhiwa

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa awali kabla ya kutokea kwa tukio hilo alikuwa na mazoea ya kumchukua mtoto huyo na kuingia naye ndani kwake na kumpatia fedha na zawadi ndogondogo ndipo siku hiyo alipofika nyumbani kwao na alimkuta mtoto peke yake alimchukua na kumfunga kitambaa usoni kisha akaingia naye ndani kwake na kumfanyia ukatili huo.

Mtoto huyo aliyefanyiwa uchunguzi na daktari na kubainika kweli ameingiliwa kimwili na kwa sasa yupo katika hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure akiendelea kupata matibabu na uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi wa polisi Augustino Senga anetoa wito akiwataka wakazi wa mwanza kuwa makini wakati wote na watoto wadogo, na kusema kuwa wasiachwe peke yao ili kuhepusha vitendo kama hivyo.

Source: MUUNGWANA BLOG

No comments:

Post a Comment