WATAALAMU WATEGUA BOMU LA VITA KUU YA DUNIA. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Monday, September 4, 2017

WATAALAMU WATEGUA BOMU LA VITA KUU YA DUNIA.

Wataalamu wa kutegua mabomu mjini Frankfurt, Ujerumani siku ya Jumapili walifanikiwa kutegua bomu kubwa ambalo halikuwa limelipuka ambalo liliangushwa wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Bomu hilo la tani 1.4 kutoka Uingereza liligunduliwa katika eneo la ujenzi Jumatano.

Habari hizo zilipokelewa kwa shangwe na watu zaidi ya 65,000 ambao walikuwa wamehamishwa maeneo yao kwa sababu za kiusalama baada ya bomu hilo kuteguliwa.

Hiyo ilikuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuhamishwa tangu kutokea kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia nchini Ujerumani, na shughuli hiyo ilihusisha mamia ya maafisa wa serikali.

Maeneo ambayo watu walihamishwa yalikuwa katika mtaa wa Westend, na ni pamoja na hospitali kadha, nyumba za kuwatunza wagonjwa na hata katika Benki Kuu ya Ujerumani.

Inaaminika kwamba kuna mamia ya maelfu ya mabomu ya wakati wa vita ambayo hayakulipuliwa ambayo yametapakaa kote Ujerumani.

No comments:

Post a Comment