MAJIMAJI YAPATA DILI LA MILLION 150.
Mwenyekiti wa Klabu ya Majimaji, Steven Ngonyani (kulia) na Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda wakisaini mkataba wa kuidhamini Majimaji.
KAMPUNI ya Mchezo wa Kubashiri ya Sokabet, imezinduliwa rasmi leo Jumatatu, Septemba 4, 2017 katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wanasoka wa zamani pamoja na waandishi wa habari, ilishuhudiwa kampuni hiyo ikiingia mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Majimaji ya Songea, wenye thamani ya Sh milioni 150.
Mratibu wa Sokabet, Franko Ruhinda amesema: “Tunayo furaha kuona leo hii tunazindua rasmi Sokabet ambayo itawapa fursa wadau wa kubeti kujishindia mamilioni kwa dau dogo tu watakaloweka kwenye kubashiri kwao michezo mbalimbali ikiwemo soka na ngumi.
“Lakini pia tunayo furaha zaidi kuingia mkataba na Majimaji ambapo kupitia timu hii inayoshiriki Ligi Kuu Bara, Sokabet itatangazwa kila kona na kujulikana zaidi nchi nzima.”
Naye mwenyekiti wa Majimaji FC, Steven Ngonyani alisema: “Tunashukuru udhamini huu wa Sokabet kwani utatuongezea kitu kwenye timu yetu hususan katika kujiendesha msimu mzima huu wa ligi ambao una mambo mengi, lakini pia tutaitangaza popote tuendapo.”
Aidha, Franko aliongeza kuwa kampuni hiyo ya Kitanzania inaanza ikiwa na mikakati mingi ya kusaidia jamii kwa kile ambacho kitakuwa kikipatikana kutokana na kubashiri, ambapo washiriki wanaweza kujiunga kwa kuingia katika tovuti ya www.sokabet.co.tz.
No comments:
Post a Comment