MASOMO YA JUMAPILI YA 2 YA MAJILIO. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Saturday, December 3, 2016

MASOMO YA JUMAPILI YA 2 YA MAJILIO.











MASOMO YA MISA, DISEMBA 4, 2016
DOMINIKA YA 2 YA MAJILIO, MWAKA "A'

WIMBO WA MWANZO: Isa 30:19, 30


Enyi watu wa Sayuni, Tazameni Bwana
atakuja kuwaokoa mataifa; naye Bwana
atawasikilizisha sauti yake ya utukufu
katika furaha ya mioyo yenu.


SOMO 1
Isa. 11:1 – 10
Siku ile: litatoka chipukizi katika shina la
Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi
yake litazaa matunda. Na roho ya Bwana
atakaa juu yake, roho ya hekima na
ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya
maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha
yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala
hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa
macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata
ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa
haki atawahukumu maskini, naye
atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa
adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya
kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo
yake atawaua wabaya.
Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake,
na uaminifu mshipi wa kujifungia. Mbwa-
mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo,
na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi;
ndama na mwana-simba na kimono
watakuwa pamoja, na mtoto mdogo
atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha
pamoja; watoto wao watalala pamoja; na
simba atakula majani kama ng’ombe. Na
mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la
nyoka, na mtoto aliyeachishwa atalia
mkono wake katika pango la fira.
Hawatadhuru wala hawataharibu katika
mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia
itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji
yanavyoifunika bahari.
Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese
lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za
watu, yeye ndiye ambaye mataifa
watamtafuta; na mahali pake pa
kupumzika patakuwa na utukufu.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKATI
Zab. 72:1 – 2, 7 – 8, 12 – 13, 17. (K) 7
(K) Siku zake yeye, mtu mwenye haki
atasitawi, na wingi wa amani hata mwezi
utakapokoma.
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako,
Na mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua watu wako kwa haki,
Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
(K)
Siku zake yeye, mtu mwenye haki
atasitawi,
Na wingi wa amani hata mwezi
utakapokoma.
Na awe na enzi toka bahari hata bahari,
Toka Mto hata miisho ya dunia. (K)
Kwa maana atamwokoa mhitaji aliapo,
Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.
Atamhurumia aliye dhaifu na maskini,
Na nafsi za wahitaji ataziokoa. (K)
Jina lake na lidumu milele,
Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao;
Mataifa yote na wajibariki katika yeye,
Na kumwita heri. (K)


SOMO 2
Ru. 15:4 – 9
Ndugu zangu, yote yaliyotangulia
kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha
sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko
tupate kuwa na tumaini. Na Mungu
mwenye saburi na faraja awajalie dunia
mamoja ninyi kwa wingi, kwa mfano wa
Kristo Yesu; ili kwa moyo mmoja na kwa
kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu,
Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi,
kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili
Mungu atukuzwe. Kwa maana nasema, ya
kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa
agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya
Mungu, kusudi azithibitishe ahadi
walizopewa baba zetu; tena ili Mataifa
wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema
zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo
nitakushukuru kati ya Mataifa, name
nitaliimbia jina lako.


SHANGILIO
Lk. 3:4, 6
Aleluya, aleluya,
Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni
mapito yake, na wote wenye mwili
watauona wokovu wa Mungu.
Aleluya.


INJILI
Mt. 3:1 – 12
Siku zile aliondokea Yohane Mbatizaji
akihubiri katika nyika ya Uyahudi,na
kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa
mbinguni umekaribia. Kwa sababu huyo
ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema,
Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni
njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Naye Yohane mwenyewe alikuwa na vazi
lake la singa za ngamia, na mshipi wa
ngozi kiunoni mwake; na chakula chake
kilikuwa nziige na asali ya mwitu. Ndipo
walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi
wote, na nchi zote za kandokando ya
Yordani; naye akawabatiza katika mto wa
Yordani, huku wakiziungama dahmbi zao.
Hata alipoona wengi miongoni mwa
Mafarisayo na Masadukayo wakiujia
ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa
nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi
kuikimbia hasira itakayokuja? Basi zaeni
matunda yapasayo toba; wala msiwaze
mioyoni mwenu kwamba, Tunaye Baba,
ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya
kwamba Mungu aweza katika mawe haya
kumwinulia Ibarahimu watoto. Na shoka
limekwisha kuwekwa penye mashina ya
miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri
hukatwa na kutupwa motoni. Kweli mimi
nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba;
bali yeyey ajaye nyuma yangu ana nguvu
kuliko mimi, wala sistahili hata
kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza
kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Ambaye
pepeto lake li mkononi mwake, naye
atausafisha sana uwanda wake; na
kuikusanya ngano yake ghalani, bali
makapi atayateketeza kwa moto
usiozimika.
Neon la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

No comments:

Post a Comment