ZAIDI YA KAYA 3,000 SUMBAWANGA ZIPO HATARINI. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Sunday, November 20, 2016

ZAIDI YA KAYA 3,000 SUMBAWANGA ZIPO HATARINI.

Kaya zaidi ya 3,400 kwenye manispaa ya Sumbawanga yenye kaya zaidi ya 47,000, hazina vyoo kabisa hali inayowaweka wakazi wa mji huo kwenye hatari kubwa kiafya, na kusababisha watu zaidi ya 5,000 kila mwezi kukumbwa na Magonjwa ya kuhara yanayosababishwa na uchafu.


Afisa afya wa manispaa ya Sumbawanga Bw. Oswald Temba, akiongea kwenye maeneo ya Soweto katika kata ya chanji wakati wa maadhimisho ya siku ya kunawa mikono, amesema licha ya kaya hizo kukosa vyoo kabisa, lakini katika ukaguzi wa nyumba kwa nyumba wamebaini kuwa zaidi ya kaya 23,600 zina vyoo visivyoridhisha, na kwamba kwa kushirikiana na asasi isiyokuwa ya kiserikali ya mazingira ya kaeso, wanatoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwa na vyoo bora kwa afya.

Akiongea na wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo, diwani wa kata ya chanji Bw. Norbert Yamsebo amesema kuna umuhimu wa halmashauri hiyo kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana wakazi wa mji huo kuhusu suala zima la usafi, ikiwa ni pamoja na utupaji wa makaratasi ovyo na taka ngumu nyingine na kula miwa ovyo mitaani.

No comments:

Post a Comment