Wadau wa mapambano dhidi ya ukimwi mkoa Simiyu wameazimia kila mjamzito anapoanza kuhudhuria kliniki lazima aende na mwenza wake ili wote wapimwe virusi vya ukimwi ikiwa ni mkakati wa kupunguza ushamiri wa maambukizi na kwamba mjamzito asipofanya hivyo hatopata huduma za kliniki.
Wadau hao ambao wamekutana kwa muda wa siku tatu wamesema kuwa azimio la kupima VVU kwa mke na mume wakati wa kipindi cha ujauzito ni moja ya mkakati ambao utaondoa ukakasi kwa wanaume wengi ambao wamekuwa wakikataa kuambatana na wenza wao katika kipindi cha kliniki kwa kisingizio cha kazi nyingi baadhi wamekuwa wakiamini kuwa iwapo mmoja akipimwa na kukutwa hana maambukizi yoyote basi wote watakuwa salama.
Akizindua rasmi mpango mkakati wa mkoa wa simiyu kwa niaba ya mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya ya itilima benson kilangi amewataka wadau hao kuwa mabalozi katika jamii kwa kuihimiza iwe na utamaduni wa mara kwa mara wa kupima kwa hiari badala ya kipindi cha ujauzito pekee.
Maazimio hayo saba yamelenga kumaliza maambukizi na hatimaye kufikia sifuri tatu ambapo maazimio hayo yanahimiza tohara kwa wanaume,viongozi wa dini kutoa elimu kwa waumini wao na mikutano ya hadhara na mikusanyiko mbalimbali ngazi ya vijiji,huku halimashauri zikitakiwa kutenga bajeti kwa ajili ya mapambano dhidi ya ukimwi.
No comments:
Post a Comment