AFUNGWA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MTOTO WAKE. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Tuesday, November 29, 2016

AFUNGWA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MTOTO WAKE.

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kongwa   imemuhukumu kifungo cha miaka  30 jela, Lazaro Madeha (56) kwa kupatikana na hatia ya  kujaribu kumbaka mtoto  wake wa kambo wa miaka tisa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo,   Marry Senapee   alisema   Mahakama yake ilijiridhisha na ushahidi uliotolewa.

Alisema ndiyo sababu imetoa adhabu hiyo  iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za ukatili kwa watoto wadogo.

Awali,  Mwendesha mashtaka wa    Polisi, Mkaguzi msaidizi, Kandoro Babile  alidai  mtuhumiwa alitenda kosa hilo Juni 26 mwaka huu   katika Kijiji cha Mkoka wilayani Kongwa.

Alidai mtuhumiwa alimkamata  mtoto huyo na kumuingiza chumbani kwake.

“Baada ya mtuhumiwa huyo kumuingiza mtoto huyo wa kambo  chumbani kwake alimvua nguo zote huku naye akiwa mtupu na kutaka kumbaka.

“Mtuhumiwa Madeha alikuwa anataka kumbaka mtoto huyo baada ya mama wa mtoto kwenda kisimani kuchota maji  na
aliporudi alimkuta mtuhumiwa akiwa mtupu kitandani  yeye pamoja  na mtoto akitaka kumbaka.

“Mama huyo alipiga kelele na majirani walifika na kumkamata,”alisema.

Mwendesha mashitaka   aliiomba Mahakama kumpa adhabu kali mtuhumiwa iwe fundisho kwa wengine weye tabia kama hizo.

No comments:

Post a Comment