WAZAZI WAASWA KUWAPELEKA HOSPITALI WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Tuesday, October 25, 2016

WAZAZI WAASWA KUWAPELEKA HOSPITALI WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI.

Wito umetolewa kwa jamii na wazazi wenye watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi kuacha kuwaficha watoto hao na badala yake kuwapeleka mapema hospitali kupata matibabu.

Ni mama wa mtoto Daniella Palanjo ambaye alimzaa akiwa na matatizo ya kichwa kikubwa, katika maadhimisho ya siku ya matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani akitoa rai kwa wazazi wenye watoto ambao wana tatizo kama la mwanawe kuachana na dhana potofu na kuwaficha ndani watoto wao kwa kufikiri kuwa kuzaa mtoto mwenye tatizo hilo ni laana badala yake kujitokeza mapema hospitali ili kupata matibabu.

Kwa mujibu wa hospitali ya mifupa MOI watoto 4000 huzaliwa wakiwa na matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi kila mwaka hivyo ili kupunguza idadi hiyo ya watoto kuzaliwa wakiwa na matatizo haya wataalamu wa afya wanashauri ni vyema kina mama wajawazito wakazingatia lishe kwa kula vyakula vyenye Folic Acid kama mbogamboga na matunda huku jamii ikitakiwa kushirikiana kusaidia matibabu ya watoto hawa.

No comments:

Post a Comment