DC MANYONI AIFUTA KAULI YAKE MWENYEWE. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Sunday, October 23, 2016

DC MANYONI AIFUTA KAULI YAKE MWENYEWE.


Siku moja baada ya mkuu wa mkoa wa Singida kufuta amri halali ya mkuu wa wilaya ya Manyoni ya kuchangia shughuli za maendeleo na inayo wataka wakazi wote wenye umri wa miaka kumi na nane kuchangia shililingi elfu kumi na tano kwa mwaka,mkuu wa wilaya ya Manyoni naye amefuta rasmi amri yake aliyoitoa Septemba sita mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa wilaya ya Manyoni Bwana Geofrey Mwambe amesema amri hiyo ambayo ilitolewa mwaka 2013 na mkuu wa wilaya aliye kuwepo awali  na yeye kuamua kuitekeleza,ameifuta rasmi baada ya agizo la mkuu wa mkoa wa Singida kufuta amri hiyo. 

Katika hatua nyingi Bwana Mwambe amesema taarifa zilizotolewa katika mitandao ya kijamii ni uzushi na yeye na wakurugenzi wake hawajawahi kupokea malalamiko ya mtu kulazimishwa kuchangia shuguli za maendeleo au kupewa adhabu ya kufungwa.

Octoba 21 mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe alitoa taarifa kwa vyombo vya habari ya kumwagiza mkuu wa wilaya ya Manyoni Bwana Geoffrey Mwambe  kufuta amri inayo husu wakazi wa wilaya ya Manyoni kuchangia pesa kwa ajili ya shuguli za maendeleo. 

No comments:

Post a Comment