SIMBA 5-0 HARD ROCK ‘LIVE’, KIPINDI CHA PILI, MCHEZO WA KIRAFIKI, UWANJA WA UHURU - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Sunday, September 3, 2017

SIMBA 5-0 HARD ROCK ‘LIVE’, KIPINDI CHA PILI, MCHEZO WA KIRAFIKI, UWANJA WA UHURU


Dakika ya 72: Simba wanajipanga tena kwa mashambulizi lakini Hard Rock kwa sasa wanaonyesha kuwa makini zaidi.

Dakika ya 61: Simba wanasogea langoni mwa Hard Rock lakini wanakuwa wameotea.

Ndemla anafunga bao la kiwango cha daraja la A, ametamba ana mpira kutoka eneo la katikati ya uwanja, akamtoka beki wa Hard Rock na kupiga shuti la mbali, likajaa wavuni.

Dakika ya 59: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!

Dakika ya 58: Simba wameutawala mchezo muda mwingi.

Kiungo mkongwe Mwinyi Kazimoto anafunga bao zuri kwa shuti kali la nje ya eneo la 18.

Dakika ya 55: GOOOOOOOOOOOOOOO!

Dakika ya 50: Simba wanamiliki mpira.

Simba wanapata bao zuri la tatu kupitia kwa Gyan ambaye anafunga akimalizia kazi nzuri ya Mo.

Dakika ya 48: GOOOOOOOOOOOOOOOO!

Dakika ya 45: Simba wamefanya mabadiliko, ametoka Luizio ameingia Nicholaus Gyan.

Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.

MAPUMZIKO

Dakika ya 47: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.

Dakika ya 46: Hard Rock wanapata kona, inapigwa na kipa wa Simba anaudaka mpira.

Dakika ya 45: Faulo kuelekea kwa Simba, Mo anacheza vibaya katikati ya uwanja.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.

Dakika ya 38: Simba wanamiliki mpira muda mwingi.

Simba wanapata bao la pili mfungaji ni yuleyule, Mo amemalizia kazi nzuri iliyoanzia kwa Ndemla kisha Luizio.

Dakika ya 36: GOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 30: Kasi ya mchezo ni ya wastani.

Dakika ya 25: Mavugo anapata nafasi nyingine akiwa yeye na kipa anashindwa kufunga, anakaa chini akiwa haamini macho yake.

Dakika ya 20: Mchezo unaendelea kwa timu zote kumiliki mpira kwa zamu lakini zaidi mchezo umebalansi.

Dakika ya 15: Simba wanaongoza bao 1-0.

Pasi nzuri kutoka kwa Said Ndemla inamfikia Mohamed Ibrahim 'Mo' anamchambua kipa.

Dakika ya 11: GOOOOOOOOOOOOOOOOO!

Dakika ya 5: Simba ndiyo wanamiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya 2: Straika wa Simba, Laudit Mavugo anakosa nafasi ya wazi akiwa yeye na lango, shuti lake linapaa juu.

Dakika ya 1: Simba wanaanza kwa kasi ndogo.

Mchezo umeanza.

Timu zote zimeishaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo.

Huu ni mchezo wa kirafiki kati ya Hard Rock ya Pemba ambao ni wageni wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru.

No comments:

Post a Comment