RAIS MAGUFULI ALIPONGEZA JESHI LA TANZANIA KUTIMIZA MIAKA 53. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Friday, September 1, 2017

RAIS MAGUFULI ALIPONGEZA JESHI LA TANZANIA KUTIMIZA MIAKA 53.

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dk. John Magufuli amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake na kwa kutimiza wajibu wake jambo ambalo limeifanya Tanzania kuwa nchi ya amani.

  

Salamu za pongezi za Rais Magufuli amezitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika, “Nalipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake. Kwa kipindi chote hiki Jeshi letu limeendelea kutimiza wajibu wake akiwa ni pamoja na kulinda amani ya nchi yetu kwa uzalendo, umahiri, ushupavu, uadilifu na nidhamu ya hali ya juu na hivyo kujijengea heshima ndani na nje ya nchi yetu. Najivunia kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa JWTZ. Mungu ibariki Tanzania, Mungu libariki Jeshi letu.”


No comments:

Post a Comment