MAHAKAMA YAFUTA USHINDI WA UHURU KENYETTA. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Friday, September 1, 2017

MAHAKAMA YAFUTA USHINDI WA UHURU KENYETTA.

Mahakama ya juu nchini Kenya imefuta ushindi wa Rais Uhuru Kenyata kwa uchaguzi uliofanyika Agosti 8, 2017, na kutaka uchaguzi huo urudiwe.

Hukumu hiyo imetolewa leo na jopo la majaji 6 ilirushwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari nchini Kenya, imesema uchaguzi huo utarudiwa baada ya siku 60.

Akisoma uamuzi huo Jaji Mkuu David Maraga amesema tume ya uchaguzi ilikiuka Katiba na Sheria katika baadhi ya mambo na hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi.

"Uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8 mwaka 2017, haukuandaliwa kwa mujibu wa katiba na sheria hivyo matokeo yake ni batili. Natangaza kwamba Bw Kenyatta hakuchaguliwa na kutangazwa kwa njia inayofaa, agizo linatolewa na kuagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa na kufanyisha uchaguzi mwingine kwa kufuata katiba na sheria katika kipindi cha siku 60", alisema Jaji Maraga.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Agosti 26 mwaka 2017 baada ya Muunganiko wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA) kuishtaki Tume ya Uchaguzi kufanya udanganyifu juu ya uchaguzi huo uliompa ushindi Uhuru Kenyata.

No comments:

Post a Comment