RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI HUU LEO. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Tuesday, April 4, 2017

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI HUU LEO.

Profesa Kitila Mkumbo ameteuliwa  kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Profesa Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi alisema katika taarifa yake iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari kuwa Profesa Kitila aliyekuwa anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.

Kitila alikuwa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Pia Rais Magufulia amemteua Dk Ave Maria Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia ambaye anajaza nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Dk Leonard Akwilapo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Kutokana na Dk Akwilapo kupandishwa kuwa katibu Mkuu wa wizara hiyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarishi amehamishwa na kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Mussa Uledi ambaye nafasi yake imetenguliwa.

No comments:

Post a Comment