WATUMISHI WATATU WATUMBULIWA KWA UTORO. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Monday, March 6, 2017

WATUMISHI WATATU WATUMBULIWA KWA UTORO.

Baraza la madiwa la halmashauri ya mkalama mkoani Singida kwa kauli moja wamewafukuza kazi watumishi watatu wa idara mifugo na uvuvi,afya na elimu  kwa kosa la utoro kazi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya mkalama Mheshimiwa James Mkwega amesema hayo kwenye kikao cha Baraza la halmashauri hiyo,na kuwataja watumishi hao ni Bwana James Kidumo Moses aliyekuwa Afisa mifugo na uvuvi daraja la tatu,Bi,sera Ogoti Afisa Muuguzi Msaidizi daraja la pili na Isa Selemani Mtunga fundi sanifu maabara wote hao wamefukuzwa kwa  kosa la utoro kazini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama  Mhandisi Godfrey Sanga amesema halmashauri yake imemteua Bwana Godluck Mlau  kuwa Kaimu Ratibu wa TASAF wilaya ya Mkalama baada ya aliyekuwepo Bwana Athumani Dule kukutwa na tuhuma za kuongeza kaya zisizo na sifa ishirini nanane.
Awali akisoma bajeti ya mpango wa makisio ya maendeleo kwa  mwaka wa fedha  2017/2018 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bwana  Loth dia  amesema Halmashauri ya Mkalama inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 18.9.

No comments:

Post a Comment