MASOMO YA DOM. YA PILI YA MWAKA "A" WA KANISA. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Friday, January 13, 2017

MASOMO YA DOM. YA PILI YA MWAKA "A" WA KANISA.



MASOMO Y AMISA, JANUARI 15, 2017
DOMINIKA YA 2 YA MWAKA A WA KANISA
WIMBO WA MWANZO: 
Zab. 66:4
Ee Mungu, nchi yote itakusujudia na kukuimbia, naam, italiimbia jina lako, wewe Mtukufu.
SOMO 1
Isa. 49:3, 5 – 6
Bwana akaniambia; Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika wewe nitatukuzwa.
Na sasa Bwana sema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee yakobo tena, na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya Bwana, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu); naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 40:1, 3, 6 – 9 (K) 7, 8
(K) Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja, kuyafanya mapenzi yako.
Nalimngoja Bwana kwa saburi,
Akaniinamia akakisikia kilio changu.
Akatia wimbo mpya kinywani mwangu
Ndio sifa zake Mungu wetu. (K)
Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,
Masikio yangu umeyazibua,
Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Ndipo niliposema, Tazama nimekuja. (K)
Katika gombo la chuo nimeandikiwa,
Kuyafanya mapenzi yako,
Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu;
Naam, sheria yako imo moyoni mwangu. (K)
Nimehubiri habari za haki
Katika kusanyiko kubwa,
Sikuizuia midomo yangu;
Ee Bwana, unajua. (K)
SOMO 2
1Kor. 1:1 – 3
Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu. Neema na iwe kwenu na Amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Yn. 12:13b
Aleluya, aleluya,
Walisema, ndiye mbarikiwa, mfalme ajaye kwa jina la Bwana,
Aleluya.



INJILI
Yn. 1:29 – 34
Siku ya pili Yohane Mbatizaji amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu; ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. Tena Yohane akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo

No comments:

Post a Comment