SERIKALI YAKOPA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 900 ILI KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI NCHINI. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Tuesday, November 1, 2016

SERIKALI YAKOPA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 900 ILI KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI NCHINI.

Serikali inategemea kukopa dola za Marekani milioni 900 ambazo ni sawa na sh trilioni 2.080 kutoka vyanzo vya nje vyenye masharti ya kibiashara ili kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni mjini hapa na waziri wa fedha na mipango, Dk. Philip Mpango, alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya taifa 2017/18 na mwongozo wa kuandaa bajeti.

Kwa upande wake msemaji wa kambi rasmi ya upinzani wa wizara ya fedha na mipango, Mh Halima Mdee amesema kusimamishwa kwa ajira mpya kumefanya nguvu kazi iliyokuwa na uwezo wa kuzalisha kuishi kama ombaomba.

Katika kipindi cha maswali na majibu baadhi ya wabunge wameitaka serikali kueleza ni lini itaanza kutekeleza ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa iliyotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ili kutatua tatizo la ajira na mitaji kwa vijana na akina mama swali lililojibiwa na waziri wanchi, ofisi ya waziri mkuu, sera bunge kazi, ajira vijana na walemavu.

Suala la uhaba wa madawa, mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nalo likaibuka ambapo baadhi ya wabunge wameomba muongozo yajadiliwe kwa dharura lakini likagonga mwamba baada ya mwenyekiti wa bunge kudai kuwa mawaziri wanayashughulikia.

No comments:

Post a Comment