SCORPION AONGEZEWA SHITAKA JINGINE. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Wednesday, November 30, 2016

SCORPION AONGEZEWA SHITAKA JINGINE.

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP)  amemuongezea shtaka lingine mshtakiwa Salum Njwete maarufu kama Scorpion na sasa atakuwa na mashtaka mawili  ya unyang'anyi wa kutumia silaha na shtaka la kujeruhi.

Scorpion aliongezewa shtaka hilo jana na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, kabla ya kumsomea Maelezo ya Awali (PH).

Baada ya kusomewa maelezo ya awali,  Scorpion alikubali hoja mbili na sita kuzikana.

Kutokana na maelezo hayo, hakimu mkazi wa mahakama hiyo,  Flora Haule aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 14, mwaka huu kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.

Mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na moja ya shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana.

No comments:

Post a Comment