POLISI WAWATAYANYA WAVUVI KWA MABIMU MABOMU YA MACHOZI. (MWANZA) - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Thursday, November 3, 2016

POLISI WAWATAYANYA WAVUVI KWA MABIMU MABOMU YA MACHOZI. (MWANZA)

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limelazimika kutumia mabomu ya machozi kwa ajili ya kuwahamisha kwa nguvu zaidi ya wavuvi 160 wanaotumia eneo la mita 60 kutoka ndani ya ziwa Victoria kufanya shughuli za uvuvi, waliopo katika mtaa wa Capripoint maji kata ya Nyamagana jijini Mwanza huku watu kumi wakishikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

ITV imeshuhudia ujenzi wa uzio unaofanywa na mkazi wa jijini Mwanza Rashid Said katika kiwanja namba 141 kitalu W, Capripoint, ambao unalalamikiwa na wakazi wanaoishi eneo hilo kwamba utasababisha kufungwa kwa njia inayotumiwa na wanafunzi wanaosoma shule ya msingi Nyamagana.

No comments:

Post a Comment