WANAOKULA CHAKULA KIBICHI WAPO HATARINI KUUGUA KICHOCHO, MINYOO NA MATENDE. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Saturday, October 22, 2016

WANAOKULA CHAKULA KIBICHI WAPO HATARINI KUUGUA KICHOCHO, MINYOO NA MATENDE.

Watu milioni 47 nchini wapo katika hatari
ya kupata magonjwa ambayo yalikuwa
hayapewi kipaumbele yakiwemo
Minyoo,Matende na Kichocho, Aidha watu
milioni 12.5 wapo hatarini kupata ugonjwa
wa Trakoma huku milioni 4 wakiwa
hatarini kupata ugonjwa wa Usubi.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam
na Ofisa mpango wa kudhibiti magonjwa
ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele
(NTD), Oscar Kaitaba kutoka Wizara ya
Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, wakati akitoa mafunzo kwa
waandishi wa habari juu ya mpango wa
taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele.
Kaitaba amesema kuwa katika wagonjwa
milioni 47 waliopo hatarini kupata
matende, kichocho na minyoo, watu
ambao wapo hatarini kupata ugonjwa wa
minyoo ni wale ambao wanakula chakula
ambacho hakijaiva.
Kaitaba ameongeza kuwa katika mpango
wa kudhibiti magonjwa hayo, Oktoba 25
hadi 30 mwaka huu katika mkoa wa Dar
es Salaam kutakuwa na ugawaji wa dawa
za kingatiba za Minyoo ya tumbo
,matende na mabusha ambazo zitatolewa
katika vituo maalum vilivyoteuliwa.
“Vituo hivyo ni pamoja na Stendi za
mabasi , masoko, hospitali, ofisi za
serikali za mitaa, ofisi za Wizara, taasisi
na kambi za jeshi na magereza,”alisema
Kaitaba.
Alitaja aina za dawa kinga ambazo
zitatolewa kuwa ni Albendazole na
Ivermectim na kwamba walengwa ni
wananchi wote kuanzia miaka mitano na
kuendelea isipokuwa wajawazito na watu
ambao ni wagonjwa mahututi. Aidha
Kaitaba alisema wanatarajia kufanya
upasuaji kwa watu 400 wenye mabusha
katika manispaa ya Ilala ambao
utafanyika katika Hospitali ya Pugu
Kajiungeni hivi karibuni.

SOURCE: MTEMBEZI BLOG.

No comments:

Post a Comment