MIFUGO 5,928 imekufa mkoani hapa katika kipindi cha kuanzia Septemba 2016 hadi Februari mwaka huu kutokana na tatizo la ukame linaloukabili mkoa huo.
Ofisa Mifugo mkoa wa Shinyanga, Beda Chamadata, akitoa taarifa ya hali ya mifugo jana alisema katika kipindi hicho ng’ombe waliokufa ni 5,855 na mbuzi ni 73.
Chamadata alisema wilaya ambayo inaongoza kwa idadi ya vifo vingi vya mifugo ni Kishapu 3,793, Kahama 2,112 na Shinyanga vijijini ni 23.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba, alisema kutokana na kuwepo kwa mabadiliko hayo ya tabia nchi amezungumza na wafugaji wilayani humo kupunguza idadi ya mifugo.
No comments:
Post a Comment