KIJANA HEMEJI ANG'OLEWA MENO NA WAFUGAJI LINDI. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Thursday, November 24, 2016

KIJANA HEMEJI ANG'OLEWA MENO NA WAFUGAJI LINDI.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi ameahidi kuunda kamati kwa ajili ya ufuatiliaji wa migogoro baina ya wafugaji na wakulima wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi na kusababisha uvunjifu wa amani na kusababisha kijana Hemedi Mwendele,Mkazi wa Kitongoji cha Ngoroma kata ya Somanga kungíolewa meno na baadhi ya wafugaji kutokana na kupigwa fimbo mara baada ya kuzuia mifugo kula shambani kwake.

Wakitoa kero zao katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa mkoa huyo,wakulima na wafugaji wamemuomba kiongozi huyo kusaidia kutatua migogoro hiyo kabla ya msimu wa kilimo, ambapo pia wakazi wa kata hiyo wametoa msisitizo wa kutaka kuondolewa kwa wafugaji hao.

Pamoja na kupokea taarifa ya Afisa mifugo wilaya ya Kilwa,Ramadhan Hatibu,Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey zambi amewataka Viongozi wa Halmashauri na kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Kilwa kufuatilia kwa kina mgogoro huo ulionza kuchochea vurugu , ambapo pia ameahidi kuunda tume itakayoongozwa na mwakilishi wa mkoa kabla ya kutoa maamuzi.

Akiwa katika ziara ya siku 3 wilayani Kilwa,Mkuu wa mkoa amefanya mikutano ya hadhara katika Tarafa 5 kati ya 6 za wilaya hiyo, ambapo alipata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya,maji na elimu katika kata za Kibata,Njinjo,Somanga,Pande na Nangurukuru iliyo mamlaka ya mji mdogo wa kivinje Singino

No comments:

Post a Comment