SERIKALI YAKUBALI KURUDISHA SH. 8,500/= KWA SIKU KWA POSHO YA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU NCHINI. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Friday, October 21, 2016

SERIKALI YAKUBALI KURUDISHA SH. 8,500/= KWA SIKU KWA POSHO YA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU NCHINI.

Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetuliza hasira za wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kurejesha posho ya chakula na malazi ya Sh8,500 kwa kila mmoja na kwamba tofauti baina yao itakuwa viwango vya ada.

Ufafanuzi huu uliotolewa jana usiku na Waziri wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza katika mahojiano maalimu na kituo cha runinga cha Taifa -TBC utakuwa faraja kwa wanafunzi ambao chini ya Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) walipanga kushinikiza walipwe posho ya Sh8,500 kwa siku kama ilivyokuwa awali.

Hatua ya wanafunzi kujenga umoja ili kushinikiza haki katika posho ilitokana na baadhi yao kuingiziwa kati ya Sh40,000 na 70,000 badala ya Sh 510,000, hali ambayo ilizua sintofahamu.

Ndalichako alisema tofauti ya malipo itakuwa katika ada na siyo posho, “Vigezo vya mikopo vimebadilika, kila mwanafunzi atapata fedha tofauti lakini tumefanya marekebisho kwenye posho ya chakula ambayo kila mwanafunzi atalipwa Sh8,500 kama awali.”

Kwa mujibu wa utaratibu wa Bodi hiyo, malipo hayo ya chakula na malazi hutolewa kila baada ya miezi miwili.

Mapema jana, Daruso iliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutotia saini fomu za fedha za mikopo yao mpaka itakapowapa ruhusa ya kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment