RAIS MAGUFULI ASAINI SHERIA YA HABARI. - KABONGE BLOG.

Blog hii ni kwaajili ya masuala/taarifa za kidini na matukio yanayotokea kila siku.

Breaking

Thursday, November 17, 2016

RAIS MAGUFULI ASAINI SHERIA YA HABARI.

John Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge katika mkutano wake wa tano mjini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa ilmeeleza kuwa Rais Magufuli amesaini sheria hiyo jana tarehe 16 Novemba 2016  na kuwapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwake.

Novemba 4 mwaka huu Rais Magufuli katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari nchini alisema kuwa mara tu sheria hiyo itakapofikishwa kwake ataisaini mara moja.

Rais Magufuli alisema hayo huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa habari nchini wakiomba muda kupitia sheria hiyo na kutoa maoni yao.


No comments:

Post a Comment